1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

HRW: Macron na Tshisekedi wazipe kipau mbele haki

3 Machi 2023

Shirika la Human Rights Watch limetoa wito kwa Marais Felix Tshisekedi na Emmanuel Macron kujadili juu ya suala la haki za binadamu watakapokutana Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4OEHn
Frankreich, Paris | Pressekonferenz mit Félix Tshisekedi und Emmanuel Macron
Picha: Giscard Kusema/Presse- und Kommunikationsdienst Kongo-Präsidentschaft

Aidha, Human Rights Watch imewataka viongozi hao kujadili pia kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba nchini Kongo, kuwalinda raia katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na kuwawajibisha wote waliohusika na vitendo vya unyanyasaji.

Hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia sio ya kuridisha kutokana na mizozo ya ndani, ufisadi na utawala mbaya. Masuala yote hayo yamechangia kukithiri kwa unyanyasaji, misukosuko ya kisiasa na kuwafanya zaidi ya watu milioni 5.8 kukosa makaazi.