1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Hakuna haki kwa washukiwa wa mauwaji Eswatini

2 Novemba 2021

Shirika la utetezi wa haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema serikali ya Eswatini inapaswa kuhakikisha maafisa wa usalama waliohusika na ukandamizaji wa watu katika maandamano ya Juni 2021 wanawajibishwa.

https://p.dw.com/p/42Sro
Eswatini | Protestierende in Mbabane zielen auf einen Militärhubschrauber
Picha: Adrian Kriesch/DW

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya iliypewa jina la "Hakuna Haki kwa mauwaji ya Juni ya waandamanaji." mi kwamba pamoja na uwepo wa wasiwasi kutoka katika kamisheni ya Umoja wa Mataifa yenye dhima na haki za binaadamu, kwamba vikosi vya usalama vimetumia risasi za moto pamoja na matumizi ya nguvu ya kupita kiasi, lakini shirika la Human Rights Watch limeweza kubani kwamba hakuna yeyote katika vikosi vya usalama nchini humo ambae amefikishwa katika mikono ya sheria.

Na kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Haki za Binaadamu ya Eswatini, ambayo ilitolewa Oktoba 29, takribani watu 46 waliuwawa katika maandamano ya Juni, wengine 245 walijeruhiwa kwa risasi na 22 waliweza kubanika na jeraha zaidi ya moja la risasi mwilini. Kadhalika katika mkasa huo pia wapo watu 118 ambao walibainikuwa kuwa na majeraha ambayo chanzo chake hakikuweza kubainika.

Waathirika wametoa wamsema wamepigwa risasi na vikosi vya usalama.

Eswatini | Protestierende in Mbabane konfrontieren die Polizei
Maafisa wa usalama EswatiniPicha: Adrian Kriesch/DW

Waathirika waliambia time huyo kwamba walipigwa risasi na wanajeshi wa Eswatini. Wakati shirika hilo la Human Rights Watch likitoa ripoti mpya yenye kujikita katika ukandamizaji wa Juni, lakini bado maandamano yameripotiwa kuendelea huku vilevile kukiwa na habari za vikosi vya usalama kutumia nguvu kubwa.

Dewa Mavhinga, ambae ni Mkurugenzi wa Human Rights Watch kwa upande wa kusini mwa Afrika anasema serikali ya Eswatini, kwa haraka inapaswa kukubali uchunguzi huru wa kimataifa kwa mauwaji hayo ya Juni pamoja na matukio mengine ya ukiukwaji wa haki za binaadamu, ambayo yametokana na matumizi ya nguvu za kupita kiasi katika operesheni za usalama wa taifa hilo.

Shirika HRW limesema Tume ya Haki za Binadamu ya Eswatini ilishindwa kutimiza wajibu wake.

Mkurugenzi Dewa anasema pamoja na kuwa na taarifa za mikasa iliyotokea Juni, lakini kimsingi Tume ya Haki za Binaadamu ya Eswatini imeshindwa kuangazia, tuhuma zote za ukizukwaji wa haki za binaadamu nchini humo kutokana na kukabiliwa na vikwazo.

Oktoba 20, Shirika Human Rights Watch lilibaini kisa cha polisi kuwafyatuliwa na risasi na mabmou ya kutoa machozi kwa waandamanaji walijaa kwenye basi ambao walikuwa wakielekea mjini Mbabane kwa ajili ya maandamano ya kupinga kufungwa kwa wabunge wawili ambao walikuwa wanapigania demokrasia. Kwa walioshuhudia mkasa huo wanasema baadhi ya abiria walijeruhiwa na kupelekwa hospitali na manusura walizuiwa kuendelea na safari ya kwenda katika maandamano.

Kwa mujibu wa Human Rights Watch, Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika SADC ambayo ilituma mjumbe wake huko Eswatini Oktoba, baada ya vurugu, ni kwamba Mfalme Mswati, ameridhia kuwepo kwa majadala wa kitaifa utakaoleta matokeo ya haki na uwajibikaji.

Chanzo: HRW