1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong yafutilia mbali pasi za usafiri za wanaharakati

12 Juni 2024

Serikali ya Hong Kong imesema imezifutilia mbali pasi za usafiri za wanaharakati sita wa demokrasia waliokimbilia Uingereza, ikiwataja kuwa "wahalifu inaowasaka."

https://p.dw.com/p/4gwn7
Hong Kong imezifutilia mbali pasi za usafiri za wanaharakati sita wa demokrasia
Hong Kong imezifutilia mbali pasi za usafiri za wanaharakati sita wa demokrasia Picha: Tyrone Siu/REUTERS

Msemaji wa serikali hiyo amesema wanaharakati hao sita ambao wote wako kwenye orodha iliyotolewa na serikali ya wanaharakati 13 wanaotafutwa, wanajificha nchini Uingereza.

Mbali ya kufutilia mbali pasi zao za usafiri, polisi ya Hong Kong imesema kuwa mtu yeyote anayewafadhili au kufanya biashara nao, anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka saba jela.

Tangu mamlaka zipige marufuku maandamano ya kupigania demokrasia mwaka 2019, Hong Kong imezidisha kamatakamata dhidi ya wapinzani na kuweka sheria kali, ambazo wakosoaji wake kama Uingereza na Marekani wanasema, zimebinya uhuru wa kipekee iliyokuwa nao sehemu hiyo ya China.