1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hoja 11 zinazoelezea kero za Muungano wa Tanzania

24 Agosti 2021

Hoja 11 kuhusu kero za Muungano zimepatiwa ufumbuzi katika kikao cha pamoja kati ya mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar cha kutatua kero za Muungano.

https://p.dw.com/p/3zR9u
Tansania Präsidentschaftswahl Nationalflagge
Picha: DW/M. Khelef

Hoja hizo 11 zimetatuliwa huku hoja tisa zikiwa zimetengenzewa hati za makubaliano ya pande mbili hizo na hoja mbili hazikuwa na hati kwa kuwa zinaweza kutekelezeka.

Hoja ambazo zimetengenezewa hati hii ni pamoja na Bahari kuu, Uingizaji wa maziwa kutoka Zanzibar, Ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano, Mgawanyo wa misaada inayotoka nje. 

Hoja nyingine ni Mkataba wa mkopo wa fedha za mradi wa ukarabati wa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja sita Mkataba wa mkopo wa barabara ya Chakechake hadi Wete Pemba saba , Mkataba wa mkopo wa ujenzi wa bandari ya Mpigaduri, nane Usimamizi wa ukokotoaji na usimamizi wa huduma za simu na tisa Mapato yanayokusanywa na uhamiaji kwa upande wa Zanzibar

Akizungumza katika mkutano uliorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango ambaye ni Mwenyekiti wa kamati amewafahamisha Watanzania kuwa makubaliano yaliotiwa saini yatakuwa na faida kwa pande zote mbili za muungano.

Sansibar Tansania Insel Alltag Strand
Wanafunzi wa kike wakipita ufukweni ZanzibarPicha: Gabriel Bouys/AFP/Getty Images

Madhumuni na nia ya kuwa na hayo yote ni kuuenzi na kuulinda Muungano huku akitoa wito kwa watendaji wote wa pande mbili.

Kwa upande wake makamo wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amesema tukio hilo litaongeza imani kwa wananchi katika kuzitafutia ufumbuzi kero za Muungano jambo ambalo liliwahi kutishia kwa baadhi ya watu kutaka kuvunjika kwa muungano huo.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mawaziri na makatibu wakuu pamoja na wataalamu kutoka pande zote mbili za Muungano kukaa kwa siku mbili mjini Zanzibar kuzijadili kero 18 kati ya kero 25 zilizoorodheshwa tangu mwaka 2006 ambapo tayari kero saba zikiwa zimetatuliwa. Kikao cha leo kinafuatia vikao viwili vilivyopita ambavyo kimoja kilifayika Juni mwaka 2010 na kingine Oktoba 17 mwaka jana.