1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jitihada za Zimbabwe katika kuzindua sarafu yake ya dola.

Admin.WagnerD9 Januari 2015

Mwaka 2009, Zimbabwe ililaazimika kuachana na dola yake ambayo hakuna alietaka kuitumia, na kuanza kutumia dola ya Marekani ili kuepusha kuanguka kwa uchumi wake na mfumuko wa bei wa kiwango cha juu kabisa.

https://p.dw.com/p/1EHxY
Simbabwe Obst- und Gemüsemarkt in Jambanja
Picha: Getty Images/AFP

Na sasa hakuna anaetaka kutumia sarafu zilizoingizwa kwenye mzunguko mwezi uliyopita.

Maamuzi ya kuitumia dola ya Kimarekani, kama sarafu rasmi ya nchi kama ilivyofanya Ecuador yanazusha maswali kuhusu ugavi wa fedha, sera ya fedha na hata uhuru wa taifa.

Kitendawili cha sarafu ya Zimbabwe kinabainisha pia ugumu wa kila siku wanaokabiliana nao wakati uchumi wao unapoelekea kwenye njia kama hiyo.

Noti za Marekani zinapatikana kirahisi, lakini kupata sarafu za dola ya Marekani na kuziweka katika mzunguko ni jambo tofauti

Kwa hiyo Gavana wa Benki kuu ya Zimbabwe John Mangudya alianzisha sarafu zilizopewa jina na 'bond coins' mwezi uliopita. Jina hilo limetokana na dhamana za dola milioni hamsini, zilizotolewa kwa ajili ya kuzichapisha na kuzisafirisha kutoka nchi jirani ya Afrika Kusini

Sarafu mpya hizo zipo katika viwango na thamani sawa kama senti za Marekani, lakini zinaweza kutumika Zimbabwe tu.

Tatizo ni kwamba siyo watu wengi wanaotaka kuzitumia kwa sababu wanaamini kuwa hawataweza kuwashawishi wengine kuzikubali. Wengine pia wanahofu kuwa sarafu hizo zinaweza kuwa njia ya kurudisha dola ya Zimbabwe inayoogopwa na watu wengi.

Kilio cha Ombaomba kote duniani ni ‘tafadhali bakiza chenji yoyote, lakini nchini Zimbabwe wanaweza kuwa na chaguo kuhusu hili.

Symbolbild Devisenhandel
Mfano wa sarafu ya dolaPicha: Getty Images

Katika taa za kuongoza magari kwenye mji wa Harare, Mwandishi wa shirika la Reuters alimpa ombaomba king'ang'anizi sarafu kadhaa, hatua iliopeleka kicheko kubwa na kisha kisha kuzikataa sarafu kabla ya kulifuata gari lingine.

Kelele husikika mitaani kutoka kwa wapiga debe wanaofanya kazi pamoja na madereva teksi pindi wanaporudisha chenji za sarafu kwa abiria ambao wanaamua kurudisha fedha hizi kwao.

"Tunao watu ambao hukataa kuchukua sarafu hizi kwa sababu wanasema hawataweza kuzitumia. Wanapenda sarafu ya Randi kutoka Afrika Kusini," alisema alisema Lyn Kahari, Msaidizi katika duka la kuuza mboga kwenye kitongoji cha mjini Harare.

Gavana wa Benki kuu Mangudya aliliambia gazeti la serikali la Herald wiki iliyopita, kuwa sarafu zinazokaribia thamani ya dola 2.5 millioni kati ya 10 millioni zilioagizwa ndio zipo kwenye mzunguko.

Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe Robert MugabePicha: Reuters

Alisema kuwa matumizi ya chini ya sarafu ni matokeo ya benki za kibiashara kutoagiza sarafu nyingi kutoka benki kuu.

Wasiwasi huu una mizizi yake kwenye kumbukumbu mbaya walio nayo Wazimbabwe kuhusu mfumuko wa bei, uliyofikia asilimia bilioni 500, ambapo bei za bidhaa zilikuwa zikibadilika zaidi ya mara mbili kwa siku kabla ya serikali ya Rais Robert Mugabe kuachana na sarafu ambayo ilipoteza kabisaa thamani yake.


Mwandishi:Nyamiti Kayora/RTRE

Mhariri:Iddi Ssessanga