1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Hofu yatanda juu ya kusambaa kwa UVIKO-19

29 Desemba 2022

Marekani imeungana na idadi inayoongezeka ya nchi zinazoiwekea China vizuizi baada ya Beijing kutangaza kuwa itaondoa vizuizi kuhusu safari za nje ya nchi.

https://p.dw.com/p/4LWTY
China | Passagiere mit Masken im Flughafen Peking
Picha: Kyodo/picture alliance

Marekani inachukua hatua hiyo wakati visa vya maambukizi ya UVIKO-19 vikiongezeka nchini China. Hospitali kote China zimelemewa na mripuko wa maambukizi kufuatia uamuzi wa Beijing kuondoa kanuni kali ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zimekidhibiti kirusi hicho lakini zikaathiri uchumi na kuzusha maandamano makubwa. Marekani na nchi nyingine kadhaa zimetangaza kuwa zitahitaji matokeo ya vipimo vya UVIKO kutoka kwa wasafiri wote wanaotokea China bara. Hatua ya Marekani inajiri baada ya Italia, Japan, India na Malaysia kutangaza hatua zao katika jitihada za kuepusha kuingiza katika nchi zao aina mpya ya virusi kutoka China. Halmashauri Kuu ya Ulaya inakutana leo kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO nchini China.