1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu ya Ebola yatanda katika mpaka wa Rwanda na DRC

17 Julai 2019

Raia wa miji miwili ya Goma mashariki mwa Congo na Gisenyi nchini Rwanda wamezitaka serikali za mataifa hayo mawili kuongeza vifaa vya uchunguzi wa homa ya Ebola kwenye mipaka. 

https://p.dw.com/p/3MCQ7
Ebola im Kongo
Picha: picture-alliance/dpa/S. Hayden

Siku chache baada ya kugunduliwa kisa cha kwanza cha Ebola mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, raia wa miji miwili ya Goma na Gisenyi katika nchi jirani ya Rwanda wamezitaka serikali za mataifa hayo mawili kuongeza vifaa vya uchunguzi wa homa ya Ebola kwenye mipaka ili kuzuia kuingia kwa homa hiyo nchini Rwanda. 

DW imezungumza na raia wa mji wa Goma na Gisenyi kwenye mpaka wa nchi hizo mbili wanaofanya shughuli za biashara na wamesema wana woga kufuatia uhaba wa vifaa vya kufanya uchunguzi wa Ebola hasa upande wa Congo.

Raia wanaoishi katika mji jirani wa Gisenyi nchini Rwanda Upande wao wadai kubaki imara katika kuzuia homa hii ya Ebola ambayo inaendelea kuwaua mamia ya watu mkoani Kivu Kaskazini

Kuna hofu kuwa ebola inaweza kuingia katika nchi jirani ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa mipakani.
Kuna hofu kuwa ebola inaweza kuingia katika nchi jirani ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa mipakani.Picha: Reuters/O. Acland

Huku hayo yakiarifiwa watu wanaoishi na ulemavu wanaofanya shughuli zao za biashara kupitia mpaka kati ya nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda wameonekana pia kusikitika sana na kisa hicho cha Ebola kilichothibitishwa na wizara ya afya mjini Goma. Hofu yao kubwa ni kwamba homa hiyo itaathiri pakubwa shughuli zao za mpakani.

Huduma za usafi zimeonekana kuongezwa maradufu katika mji wa Goma huku nchi jirani ya Rwanda ikiwataka pia raia wake kuheshimu kanuni za usafi ili kuzuia maambukizi yoyote ya Ebola.

Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumanne mjini Goma, wakili wa shirika la afya duniani WHO mkoani Kivu kaskazini na Ituri bwana Michel Yao alithibitisha kwamba mchungaji aliyegunduliwa na homa ya Ebola wiki hii alifariki njiani pindi alipokuwa akirejeshwa mjini Butembo.

Mwandishi: Benjamin Kasembe