1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hisia Mseto baada ya CCM kumpitisha Dr Tulia kuwania Uspika

Deo Kaji Makomba
21 Januari 2022

Siku moja baada ya Chama cha Mapinduzi CCM chini ya mwenyekiti wake, Samia Suluhu Hassan kumpitisha Tulia Ackson kukiwakilisha chama hicho katika nafasi ya uspika wa bunge hilo, kumekuwa na hisia mseto.

https://p.dw.com/p/45sdb
Tansania Dr. Tulia Ackson
Picha: Ericky Boniphace

Mtizamo mkubwa unaonekana katika macho ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania ni kwamba Rais Samia sasa kaamua kujidhatiti katika nafasi yake ya uongozi ikiwa ni pamoja na kuwapatia nafasi za juu katika serikali yake wanawake

Hatua ya Rais Samia kuteuwa wanawake katika nafasi mbalimbali za juu katika serikali yake ikiwemo wizara ya ulinzi, wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa pamoja na wizara mbalimbali ambazo zinashikiliwa na wanawake na hapo jana akiongoza kikao cha kamati kuu ya Halmashauri kuu ya taifa ya CCM kumptisha Tulia Ackson kuwania nafasi ya Uspika.

Tansania Wahl des Premierministers Kassim Majaliwa
Job Ndugai aliyejiuzulu nafasi ya spikaPicha: DW/H. Bihoga

Mbali na CCM, chama cha upinzani cha Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kimefungua mchakato huo na mwanachama wake, Maimuna Kassim amekuwa wa kwanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa nafasi ya Spika.

Hatua ya CCM chini ya mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan kumteua naibu spika wa bunge Tulia Ackson kuwania nafasi ya Uspika imepokelewa kwa hisia mseto na wana siasa pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania. 

Lakini wakati hayo yakitokea chama cha NCCR Mageuzi kupitia mwenyeki wake James Mbatia akizungumza na DW amesema kuwa tayari amekwenda mahakama kuu ya Tanzania kufungua kesi kupinga kujizulu kwa Ndugai kulikosababisha mchakato wa kumteua Tulia Ackson kugombea nafasi hiyo. Kuteuliwa kwa Tulia Ackson na chama chake cha CCM, kumeendelea kuzua mijadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii.