1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Helsinki. Viongozi wajadili kuhusu uchafuzi wa mazingira.

12 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDJ

Viongozi wa mataifa ya Ulaya na Asia wamemaliza mkutano wao mjini Helsinki kwa taarifa kuhusu hali ya ujoto duniani, biashara ya dunia na mapambano dhidi ya ugaidi.

Lakini mataifa yanayochipukia yenye nguvu katika bara la Asia, yamejizuwia kujiweka pamoja katika ahadi kamili za kupunguza gesi zinazoharibu mazingira.

Viongozi hao pia wameweka kando masuala nyeti kama masuala ya haki za binadamu nchini China na kuongezeka kwa kuhami zaidi kwa masoko ya Ulaya dhidi ya bidhaa zinazoingizwa kutoka Asia.

Mkutano huo , ulioitishwa na Finland ambayo inashikilia urais wa umoja wa Ulaya, ulihitaji kuyabana mataifa yanayoinukia ya Asia kuweza kutumia teknolojia za kupunguza gesi zinazoharibu mazingira na kuyahimiza mataifa ya magharibi kusaidia katika teknolojia inayotumia nishati kwa uangalifu.