1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEARTS OF OAK WATAWAZWA MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AFRIKA.FIFA NA UEFA KUSAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO ASIA NA KIPCHOGE AAHIDI KUMSHINDA BEKELE KATIKA MBIO ZA NYIKA HUKO UFARANSA MWEZI MACHI.

Ramadhan Ali10 Januari 2005
https://p.dw.com/p/CHZa

Mashirikisho 2 makubwa ya dimba duniani-FIFA na lile la Ulaya-UEFA yanapanga kuandaa dimba maalumu la mshikamano na nchi zilizokumbwa na maafa ya Tsunami katika Bahari ya Hindi mwezi ujao .

Shirikisho la dimba ulimwenguni-FIFA-limearifu kwamba limeanzisha mfuko maalumu pamoja na Shirikisho la dimba la Asia (AFC) na tayari mfuko huo umepokea michango .

FIFA tayari limeaahidi dala milioni 2 kwa mfuko huo na AFC-shirikisho la Asia likajitolea kuchangia dala milioni 1 kujenga upya zana za kuchezea dimba katika eneo hilo lililokumbwa na maafa.Pia litachangia mipira,jazi,viatu na zana nyengine.Mwezi uliopita zilzala iliopiga kisiwani Sumatra,Indonesia ilisababisha mawimbi makubwa na mafuriko yalioathiri Indonesia,Thailand,Sri Lanka,India hadi Somalia.

Jumla ya watu 153,000 wanakisiwa wameuwawa.

Mabingwa wa Ujerumani-Werder Bremen, wamefunga mkataba wa kumuazima mshambulizi kutoka Misri Mohamed Zidane anaeichezea klabu ya Danmark .

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 23 atajaza pengo lililoachwa kwa kuuzwa kwa stadi wa kombe la Ulaya wa ugiriki Angelos Haristeas kwa Ajax Amsterdam kwa kitita cha dala milioni 6.48.

Mkurugenzi wa Werder Bremen,Klaus Allofs amesema kwamba Bremen itakua na chaguo ama kumununua kabisa Zidane baada ya kumalizika mkataba wa sasa wa kumuazima au kumuachia kurudi klabu yake.

Werder Bremen ina miadi na Olympique Lyon katika duru ya kwanza ya kutoana ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwezi ujao.

hapo kabla ilivuma kwamba, werder ingemuajiri Shabani Nonda-nahodha wa Kongo amnaeichezea Monaco, lakini wakati huu ameumia.

Na stadi wa Ufaransa anaeichezea Real madrid Zinedine Zidane ametaja kwamba huenda akaacha kucheza dimba la malipo kabla mkataba wake na real Madrid kumalizika 2007.Zidane ambae wakati huu ana umri wa miaka unaingia miaka 33 mwezi juni mwaka huu,alijiunga na Real kwa kitita kikubwa kabisa cha dala milioni 66 hapo 2001 kutoka Juventus ya Itali.

Zidane amesema hana masikitiko kuhusu kuacha kuichezea timu ya Taifa baada ya Ufaransa kupigwa kumbo si na mwengine bali Ugiriki ilioibuka mabingwa wa Ulaya katika mashindano yale huko Ureno.

HEARTS OF OAK NA SIO ASANTE KOTOKO NDIO MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA DIMBA BARANI AFRIKA:

Hearts of Oak katika finali ya Kombe la CAF-shirikisho la dimba la Afrika iliokumbanisha klabu 2 za Ghana, Hearts og Oak iliwika nyumbani mwa asante kotoko kwa mabao 8-7 ya changamoto za mikwaju ya penalty.

Baada ya duru ya kiwanza ya finali ya kombe hili mjini Accra, wiki moja kabla kumalizika suluhu bao 1:1, jana Hearts of Oak ilivunja mzizi wa fitna katika zahama ya mikwaju ya penalty.Hearts ilisawazisha na kufaya matokeo mabao 2:2 mnamo dakika 10 za mwisho na baadae ikaitimua Kotoko nyumbani mjini Kumasi.Ilikua Kotoko iliopigiwa upatu kushinda lakini wapi, mambo yaliwaendea mwishoe kombo.Hearts of Oak,klabu kongwe kabisa ya dimba barani afrika, iliibuka pia mabingwa wa kombe la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2000.

Katika dimba la kirafiki,Misri ililazajana Uganda mabao 3:0 mjini Cairo .Serengeti Boys-timu ya chipukizi ya Tanzania,imeizaba Zimbabwe mabao 3:1 jumamosi mjini Dar-es-salaam.Mabao ya Tanzania yalitiwa na Omari Matuta alieutikisa wavu mnamo dakika ya 9 na ya 40 kabla Yusuf Mgwao kutia bao la 3 la chipikizi hao wa tanzania wanoania nafasi ya kwenda Gambia:

RIADHA:

Bingwa wa dunia wa masafa ya mita 5000,mkenya Eliud Kipchoge ametoa changamoto mwishoni mwa wiki kwa Muethiopia bingwa mara kadhaa wa mbio za nyika ulimwenguni-Kenenisa Bekele.Kipchoge ameariofu kwamba kenya ina mkakati maalumu kumshinda muethiopia huyo.Mashindano yajayo huko Ufaransa yatafanyika huko St.Gamier,Machi 19 na 20. Kipchoge alitoa ionyo hilo baada ya ushindi wake mwishonni mwa wiki katika mbio za nyika za taifa nchini kenya mjini Eldoret.