1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA : Umoja wa Ulaya wamtaka Casto kuwaachilia huru wapinzani

27 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFT9

Mkuu wa masuala ya Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Louis Michel amemtaka Rais Fidel Castro wa Cuba kuwaachilia huru wapinzani walioko magerezani.

Wakati wa mkutano wake wa maasa manne mjini Havana kiongozi huyo wa Cuba ameelezea utashi wake wa kulitafakari suala hilo na Ulaya.Ziara ya Michel ni ya kiongozi mwandamizi kabisa kuwahi kufanywa na kiongozi wa Umoja wa Ulaya tokea Cuba ilipowatia ndani takriban wapinzani 75 watetezi wa demokrasia hapo mwezi wa Machi mwaka 2003 ikiwa ni siku chache tu baada ya Umoja wa Ulaya kufunguwa ubalozi wake mjini Havana.

Kufuatia ombi la serikali mpya ya kisoshalisti nchini Uhispania Umoja wa Ulaya uliondowa vikwazo vyake vya kidiplomasia hapo mwezi wa Januari na kurudia katika sera yake ya kuzungumza na Cuba ambayo itaangaliwa upya hapo mwezi wa Juni.