1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana: Cuba inakataa kusaidiwa na Marekani na nchi za Jumuiya ya Ulaya baada ya kukumbwa na tofani

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvF

Rais Fidel Castro wa Cuba ameukataa msaada uliotaka kutolewa na Marekani na nchi za Jumuiya ya Ulaya kwa nchi yake kutokana na tufani iliotokea nchini mwake. Katika hotuba yake kupitia televisheni ya serekali alisema uharibifu uliosababishwa na dhoruba hiyo ya mawimbi makali kutoka baharini unakadiria kufikia gharama ya dola bilioni 1.4. Peke yake huko Cuba watu 16 walikufa kutokana na janga hilo. Huko Haiti watu 22 walikufa.