1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatua zaa kupambana na mabadiliko ya tabianchi Ujerumani

Oumilkheir Hamidou
17 Desemba 2019

Mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa kilele kuhusu nafasi za kazi kwa wahamiaji na vishindo vya kazi wanavyokabiliana navyo matabibu ni miongoni mwa mada zilizogonga vichwa vya habari magazetini.

https://p.dw.com/p/3Uwrk
Spanien 25. UN-Klimakonferenz in Madrid | Svenja Schulze
Picha: picture-alliance/dpa/J. Hellín

Tunaanzia Berlin ambako usemi wa waswahili "penye nia pana njia" umethibitika. Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linaandika. "Siku moja tu baada ya kumalizika bila ya mafanikio mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi mjini Madrid nchini Uhispania, Ujerumani imebainisha, katika suala la kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kila kitu kinawezekana ikiwa watu watadhamiria. Wawakilishi wa serikali kuu na wale wa majimbo wamekubaliana kuyafanyia marekebisho ya kina makubaliano kuhusu juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Hata kama mipango iliyodurusiwa bado haionyeshi  kama ina uwezo wa kupunguza moshi wa sumu unaotoka viwandani, hata hivyo lengo linalofuatwa ni hilo hilo."

Wageni wenye ujuzi wapatiwe kazi

 Serikali kuu ya Ujerumani na waajiri walikuwa na mkutano kutathmini namna ya kuwarahisishia wahamiaji wenye ujuzi, nafasi ya kupata kazi humu nchini. Gazeti la "Wiesbadener Kurier" linaandika: "Kwa kupitisha sheria ya waajiriwa wakigeni wenye ujuzi, serikali kuu ya Ujerumani imeachana hatimae na ule usemi Ujerumani si nchi ya uhamiaji. Ujerumani ni nchi ya uhamiaji kimsingi tangu miaka ya 60. Hata hivyo sheria hiyo bado ina walakin. Baadhi ya hatua ni za maana lakini  hazendi mbali sana. Na mkakati wote huo una ila pia: Lengo limefafanuliwa ipasavyo lakini jinsi ya kulitekeleza ndio kishindo."

Upungufu wa madaktari Ujerumani

 Mada yetu ya mwisho magazetini inatufikisha katika vituo vya huduma za afya ambako wauguzi na matabibu wanalalamika, kazi ni nyingi mno. Gazeti la "Berliner Morgenpost" linaandika: "Vituo vya afya vinashuhudia madhara ya uhaba wa matabibu na wauguzi katika mfumo wa afya nchini Ujerumani. Madaktari wanaoamua kufanya kazi nusu siku  au kuvihama  kabisa vituo vyao vya afya idadi yao inazidi kuongezeka . Badala yake wanajiunga na sekta nyengine za afya. Badala ya kuwapa moyo wanaokubali kufanya kazi katika hali ya shida, hakuna kinachotokea na wengine wanajionea jinsi wagonjwa wanavyoweza kujisaidia."