1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Rais Mugabe akataa mazungumzo

8 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmo

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekataa mwito wa kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

Rais Mugabe aliuhutubia umati wa watu waliokuwa wakimshangilia katika kuadhimisha siku ya kumalizika vita vya Zimbabwe dhidi ya koloni la zamani Uingereza na akasema kuwa wale wanaotaka kufanyike mazungumzo ya kutafuta suluhu baina ya viongozi hao ili Zimbabwe imalize uhasama wa kisiasa na uchumi wanapaswa kusahau ndoto hiyo.

Wadadisi wanasema kuwa hotuba ya rais Mugabe imeilenga moja kwa moja Afrika Kusini.