1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Muswada wenye utata wa sheria wapitishwa Zimbabwe.

30 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEfx

Bunge la Zimbabwe leo limeidhinisha,muswada wa sheria wenye utata ambao unaonekana kuwa na upinzani mkubwa,ambao unawazuia wakulima wa kizungu kwenda mahakamani kudai ardhi yao iliyochukuliwa na serikali.Muswada huo pia unahusu kuwapunguzia safari na haki ya kupiga kura,wale wote ambao hawana uraia kamili wa nchi hiyo.

Muswada huo wa sheria ulipitishwa kwa kura 103 dhidi ya 29 zilizopinga,katika Bunge lenye viti 150 huku chama tawala cha ZANU-PF kinachotawala cha Rais Robert Mugabe kikiwa na wabunge 107.

Akiuwasilisha muswada huo,Waziri wa Sheria wa Zimbabwe,Patrick Chinamasa,amesema marekebisho hayo yatawezesha Zimbabwe kupambana kikamilifu na mbinyo inaoupata kutoka kwa watawala wa Uingereza.

Muswada huo pia utaweza kuwatambua wale wote wenye mzazi mmoja au wote wawili raia wa kigeni ambao wanamiliki hati za kusihi za kudumu za nchi hiyo lakini hawana uraia kamili.

Chama cha upinzani cha MDC kimeupinga muswada huo na kusema kuwa chama cha ZANU-PF kinajifanyia tu mambo kadri kinavyohisi ni sawa kwao.