1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE,Mugabe aambulia dola milioni 6 tu!

2 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEoh

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimeripoti kwamba katika ziara yake nchini China, rais Robert Mugabe wa Zimbabwe hakufanikiwa kupata mkopo wa dola milioni mia tatu anazohitaji ili kulipa deni la shirika la fedha la kimataifa IMF.

Badala yake China imempa bwana Mugabe msaada wa dola milioni sita za kununulia chakula.

Zimbabwe imo hatarini kufukuzwa kutoka shirika la IMf ikiwa kama haitalipa deni hilo.

Hatahivyo Africa ya Kusini ilitangaza mapema wiki jana kuwa ipo tayari kuisaidia serikali ya bwana Bwana Mugabe lakini ya sharti kwamba inatekeleza haki za binadamu.

.