1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Upinzani nchini Zimbabwe unataka uchaguzi mpya

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQE

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kimetoa muito wa kufanywa chaguzi mpya za bunge,baada ya kupoteza theluthi moja ya viti vyake katika chaguzi zilizofanywa wiki iliyopita.Chama cha MDC kilishindwa vibaya,kikijinyakulia viti 41 tu kutoka jumla ya viti 120 vilivyogombewa.Msemaji wa MDC amesema uchaguzi huo ulikuwa "wa uwongo" kwa sababu vyombo vyote vya uchaguzi vilidhibitiwa na chama cha rais Robert Mugabe.Akasema mageuzi ya katiba yanahitaji kufanywa ili kuzuia ushawishi wa chama tawala cha Mugabe cha ZANU-PF katika kamati za uchaguzi.Chama cha ZANU-PF kimeyapinga madai ya MDC na kusema kuwa ni "upuzi mtupu."Kwa upande mwingine Umoja wa Ulaya umesema uchaguzi huo ulikuwa wa bandia,huku Marekani ikisema uchaguzi ulikuwa na dosari.