1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Rais Kikwete kutuliza mzozo wa Zimbabwe

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIo

Kumekuwa na jitihada za kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe ambapo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amekuwa katika mazungumzo na Rais Robert Mugabe mjini Zimbabwe.

Baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais John Kofour wa Ghana kukiri kwamba bara hilo limekarahishwa na kukamatwa na kupigwa vibaya kwa viongozi na wanaharakati wa upinzani nchini Zimbabwe Kikwete amewasili katika Ikulu ya nchi hiyo kwa mkutano ambao ulikuwa haukupangwa hapo awali.

Juu ya kwamba hakuna maelezo ya mkutano huo kutoka serkali ya Zimbabwe afisa wa wizara ya mambo ya nje wa Tanzania amesema Kikwete yuko katika ziara ya kutuliza mvutano kati ya serikali na chama cha upinzani cha Morgan Tsvangirai cha MDC.

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati shinikizo la kimataifa likiongezeka kwa Mugabe huku Australia ikishutumu nchi jirani na Zimbabwe kwa kutochukuwa hatua za kutosha kumdhibiti kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 83 ambaye inadaiwa kuwa ameitumbukiza nchi yake katika matatizo makubwa kabisa ya kiuchumi na kupanda kwa gharama ya maiasha kwa asilimia 1,730.