1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE. Chama cha upinzani chapongeza ripoti ya Umoja wa Mataifa

24 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErO

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Movement for Democtratic Change kimepongeza ripoti ya umoja wa mataifa inayopinga hatua ya serikali ya rais Robert Mugabe ya kuvunja makao ya mabanda mjini Harare na kuutaka umoja wa mataifa uichukulie hatua serikali ya rais Mugabe.

Ripoti hiyo kutoka mjini Newyork imetaka serikali ya Zimbabwe kusimamisha operesheni ya kuvunja makao ya mabanda hatua mabayo chama cha upinzani cha MDC kimesema imewanyima makaazi watu laki saba na kuwaathiri wengine milioni 2.4.

Chama cha upinzani kimetaja hatua hiyo ni kama adhabu kwa wakaazi hao wa mitaa ya mabanda kwa kukiunga mkono chama cha upinzani tangu kilipo anzishwa mwaka 1999.

Serikali ya rais Mugabe imekanusha madai hayo na kusema kuwa hatua hiyo ilikuwa na azma ya kupunguza makaazi ya mabanda mijini ambayo yaligeuka kuwa sehemu za kuwaficha wahalifu.