1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamdok arudishwa tena madarakani Sudan

21 Novemba 2021

Hatimae madaraka yamerudishwa kwa waziri mkuu Abdallah Hamdok atakayeunda serikali kamili ya kiraia na kuandaa uchaguzi nchini Sudan

https://p.dw.com/p/43J4V
Sudan Premierminister Abdalla Hamdok
Picha: AFP

Jeshi la Sudan limemrudisha madarakani waziri mkuu Abdalla Hamdok  leo Jumapili na kutangaza kuwaachia huru  wafungwa wote wa kisiasa waliokamatwa baada ya wiki kadhaa za machafuko yaliyochochewa na mapinduzi.
Chini ya makubaliano yaliyosainiwa leo pamoja na jenerali AbdelFatah al Burhani,Hamdok ataiongoza serikali ya kiraia ya wataalamu katika kipindi cha mpito.

Waziri mkuu huyo kwa upande wake amesema amefikia makubaliano hayo ili kumaliza  umwagikaji damu nchini Sudan. Bwana Hamdok amenukuliwa akisema-
''Damu ya Wasudan inathamani,tusitishe umwagikaji damu na tuziongoze nguvu za vijana katika ujenzi na maendeleo'' Mwisho wa kumnukuu. Lakini muungano wa kiraia uliogawana madaraka na jeshi kwenye serikali iliyokuwepo umesema unapinga mazungumzo yoyote na jeshi  na wametaka maandamano zaidi yanedelee hii leo.

Sudan Khalid Mehdi, Polizeichef spricht während einer Pressekonferenz in Khartoum
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Makubaliano hayo ya kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini Sudan yanakuja baada ya kufanyika mazungumzo marefu ya kina baina ya viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi na wawakilishi wa kiraia.

Ikimbukwe kwamba bwana Hamdok aliteuliwa waziri mkuu kuiongoza serikali ya mpito mnamo mwaka 2019 baada ya maandamano makubwa sana yaliyomuondowa madarakani kiongozi wa zamani aliyeitawala nchini hiyo kwa miongo kadhaa, Dikteta Omar al Bashir.

Serikali ya waziri mkuu Hamdok kimsingi ilipewa jukumu la kuandaa uchaguzi ujao ambao kwahakika ungelifanya jeshi kulazimika kupisha utawala kamili  wa serikali ya kiraia. Wakati wa kipindi cha mpito Sudan ilikuwa ikiongozwa na baraza huru la utawala ambalo liliwajumuisha pia wanajeshi na viongozi wa kiraia.

Sudan | Proteste nach dem Militärputsch
Picha: Marwan Ali/AP/dpa/picture alliance

 Makubaliano hayo ya utawala wa kugawana madaraka yalionekana kuvunjwa mnamo mwezi uliopita wa Oktoba pale jenerali Abdel Fattah al Burhani alipoamua kuivunja serikali na kumuweka waziri mkuu Hamdok kwenye kifungo cha nyumbani na kutangaza hali ya hatari.

Lakini Wasudan waliingia tena mitaani na kufanya maandamano ya kila uchao yaliyoshuhudia vurugu na watu 15 kuuwawa katika duru ya hivi karibuni ya maandamano hayo.Ni baada ya wanajeshi kuwashambulia kwa risasi za moto waandamanaji. 

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW