1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG : Polisi washikilia watuhumiwa watatu wa ugaidi

27 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhP

Polisi katika mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Hamburg imewakamata Wachechen watatu kuhusiana na uwezekano wa kufanya shambulio la kigaidi.

Wanaume hao walipigwa picha na kamera za uchunguzi kwenye basi mjini Hamburg hapo Jumaatano na kuja kuwa shabaha ya msako mkubwa baada ya shahidi moja kuwaambia polisi kwamba aliwasikia wakizungumzia juu ya kuwa mashujaa kwa Allah.

Polisi inasema kwa hivi sasa hawana ishara kwamba watu hao walikuwa kweli wanapanga shambulio.Watuhumiwa wawili kati yao walijisalimisha wenyewe wakati watatu alikamatwa na polisi.

Zaidi ya polisi 1,000 walimwagwa kwenye msako mjini humo Alhamisi usiku kwa kuweka vizuizi vya barabarani pamoja na kupekuwa majengo.