1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Hamas yasema haijapokea taarifa kutoka kwa wapatanishi

12 Julai 2024

Kundi la Hamas limesema kuwa wapatanishi wa mzozo kati ya Israel na kundi hilo bado hawajatoa taarifa zozote kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza.

https://p.dw.com/p/4iCtV
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kushoto) akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (Kulia) wakati wa mkutano huko Virginia, Marekani.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant (kushoto) akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (Kulia) wakati wa mkutano huko Virginia, Marekani.Picha: Michael Reynolds/EPA

Katika taarifa yake, Hamas pia imeishutumu Israel kwa mkwamo uliopo, ili kupata wakati na kuzuia duru ya sasa ya mazungumzo, kama ilivyofanya katika duru zilizopita.

Soma pia: UN yaonya kuhusu IDF kuwataka raia kuondoka Ukanda wa Gaza

Hamas imetoa matamshi hayo wakati wapatanishi wa Qatar na Misri, wakiungwa mkono na Marekani, wakiongeza juhudi wiki hii ili kukamilisha makubaliano ya kusitisha mapigano yenye lengo la kumaliza vita vya miezi tisa huko Gaza.

Pia kwa lengo la kuwaachilia huru mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas na Wapalestina wengi waliofungwa jela nchini Israel.