1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas imesema mazunguzo ya amani yana matumaini.

21 Novemba 2023

Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh amesema hii leo kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel yanakaribia, na hivyo kuongeza matumaini ya kuachiliwa huru makumi ya watu waliochukuliwa mateka Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4ZFaJ
Palästina | Der abgesetzte palästinensische Premierminister Ismail Haniyeh von der Hamas
Picha: Hatem Moussa/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Hata hivyo, Israel haijazungumza chochote kuhusu kauli hiyo.Kulingana na makubaliano hayo, Hamas itaawachilia mateka kati ya 50 na 100 huku Israel ikiwaachilia huru Wapalestina wapatao 300 na kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano.Hamas inawashikilia mateka wa Israel wapatao 240 ambao wengi wao ni watoto na wazee na hadi sasa wachache tu ndio wamefanikiwa kuokolewa na jeshi la Israel au miili yao kupatikana.Tangu kuanza kwa mzozo huu, Tel Aviv imesema watu wake 1,200 waliuawa na kulingana na mamlaka ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas, tayari mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 13,300 wakiwemo maelfu ya watoto.