1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Halmashauri ya UIaya yaidhinisha mipango ya meguzi ya Kiev

16 Aprili 2024

Halmashauri Kuu ya UIaya imeidhinisha mipango ya mageuzi ya Ukraine inayohitajika ili kutoa fedha zaidi kutoka kwa mpango wake wa msaada wa mabilioni ya euro.

https://p.dw.com/p/4ep9I
Ushirikiano wa Ukraine na Umoja wa Ulaya
Halmashauri ya Ulaya imetoa tathmini chanya ya mageuzi ya Ukraine na mkakati wa uwekezaji kwa miaka minne ijayoPicha: Bogdan Hoyaux/European Union | CC BY 4.0

Halmashauri hiyo imetoa tathmini chanya ya mageuzi mapana ya Ukraine na mkakati wa uwekezaji kwa miaka minne ijayo, hatua inayofungua njia kwa nchi hiyo iliyo chini ya uvamizi wa Urusi, kupewa msaada wa mara kwa mara.

Soma pia: Ukraine yaomba misaada ziada ya kijeshi kuikabili Urusi

Nchi za Umoja wa Ulaya sasa zina mwezi mmoja kutoa idhini kwa mpango huo, ambao utatoa hadi euro bilioni 1.89 kama ufadhili wa kabla hadi pale malipo ya kawaida yatakapoanza kutolewa. Mpango huo wa msaada wa Umoja wa UIaya, ulioidhinishwa Februari, unatoa msaada wa euro bilioni 50 kwa kipindi cha miaka minne.

Euro bilioni 33 kati ya hizi zitalipwa kama mikopo na zinazobaki zitatolewa kama ruzuku isiyohitaji kurejeshwa. Kiasi cha euro bilioni 4.5 kilitolewa mapema mwishoni mwa Machi na uzingatiaji wa masharti ulipaswa kuangaliwa kabla ya fedha zaidi kutolewa.