1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaBrazil

FAO: Zaidi ya watu milioni 23 walikabiliwa na njaa, 2022

10 Novemba 2023

Shirika la kimataifa la Chakula na Kilimo, FAO limesema karibu watu milioni 43.2 wa Amerika ya Kusini na Karibiki walikabiliwa na njaa mnamo mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/4Ye0S
Kulingana na shirika la FAO, idadi kubwa ya watu walikosa lishe inayofaa na kuibua kitisho cha aina mbalimbali za utapiamlo
Kulingana na shirika la FAO, idadi kubwa ya watu walikosa lishe inayofaa na kuibua kitisho cha aina mbalimbali za utapiamloPicha: Agostina Canaparo/DW

Idadi hiyo ni sawa na asilimia 6.5 ya watu wote kwenye eneo hilo la Amerika ya Kusini na Karibiki.

FAO limesema licha ya juhudi za maboresho ya tangu mwaka 2021, lakini idadi imeongezeka kuliko ilivyokuwa kabla ya janga la UVIKO-19, wakati watu karibu milioni sita zaidi wakikabiliwa na njaa kuanzia mwaka 2019.

Taarifa hiyo ya FAO iliyoangazia hali ya usalama wa chakula na lishe imesema changamoto hiyo ilichochewa kwa kiasi kikubwa na janga hilo la UVIKO, mzozo wa hali ya hewa, vita vya Ukraine, ukuaji hafifu wa uchumi, mfumuko wa bei za vyakula na kukosekana kwa usawa wa kipato.

Imesema mmoja kati ya watu watano kwenye ukanda huo hapati mlo kamili na kuibua kitisho cha aina zote za utapiamlo.