1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Berlusconi inaimarika

10 Aprili 2023

Madaktari wanaomtibu waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, wanasema afya yake inaimarika "hatua kwa hatua na polepole," tangu alipopelekwa hospitalini hapo na kulazwa juma lililopita.

https://p.dw.com/p/4Psbg
Silvio Berlusconi Porträt
Picha: Photoshot/picture alliance

Madaktari wanaomtibu waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, wanasema afya yake inaimarika "hatua kwa hatua na polepole," tangu alipopelekwa hospitalini hapo na kulazwa juma lililopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Hospitali ya Milan's San Raffaele, madaktari hao wanasema matumani yao yanatokana na matibabu kwenda kama yalivyotarajiwa.

Pasipo kubainisha zaidi, madaktari hao walisema utendaji wa kiungo ambacho walikuwa wakikifutalia, umekuwa ikiimarika ipasavyo katika kipindi cha masa 48 yaliyopita.

Berlusconi, mwenye umri wa miaka 86 na ambae aliongoza serikali nne za Italia kuanzia 1994 hadi 2011, Jumatano iliyopita alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na homa ya mapafu na saratani ya damu.