1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

"Barbeque" awatisha wanasiasa wanaowania uongozi

15 Machi 2024

Kiongozi wa mtandao wa magenge ya uhalifu nchini Haiti ametoa ujumbe wa vitisho kwa viongozi wa kisiasa watakaojiunga kwenye baraza la mpito la utawala, wakati hali ikizidi kuzorota katika mji mkuu wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4dXML
Haiti | Machafuko katika mji wa Port-au-Prince
Muandamanaji akichoma matairi wakati wa maandamano baada ya kujiuzulu Waziri Mkuu Ariel Henry, huko Port-au-Prince, Haiti, Machi 12, 2024.Picha: Clarens Siffroy/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo Jimmy "Barbeque" Cherizier alirekodi vitisho hivyo kwenye ukanda wa sauti wa dakika saba siku ya Jumatano na kuusambaza jana Alhamisi kupitia mtandao wa WhatsApp.

Kwenye ukanda huo Barbeque amesikika akiwaonya wanasiasa walioonyesha nia ya kujiunga na baraza hilo na juu ya kile kitakachotokea ikiwa pamoja na kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya familia zao.

Aidha amesema kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry ilikuwa ni hatua ya kwanza katika mapambano kwa ajili ya Haiti yenye karibu watu milioni 11.