1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti na Kenya zaanzisha uhusiano wa kidiplomasia

21 Septemba 2023

Haiti na Kenya zimeanzisha rasmi uhusiano wa kidiplomasia. Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa X uliokuwa Twitter zamani. na Waziri Mkuu wa taifa hilo la Caribbean, Ariel Henry.

https://p.dw.com/p/4Wd56
Sicherheit in Haiti
Picha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na mijadala ya kimataifa kuhusu uwezekano wa Kenya kuongoza kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Mataifa kusaidia polisi wa Haiti, wenye rasilimali chache, kupambana na magenge ya uhalifu ambayo yanakadiriwa kudhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Haiti inakabiliwa na changamoto ya makundi ya wahalifu wanaosumbua raia na hasa katika mji mkuu, Port-au-Prince

Mapema wiki hii, afisa mmoja wa Marekani alisema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza ndani ya muda wa wiki moja, kupiga kura kuidhinisha kikosi cha kimataifa kwa ajili ya Haiti. 

Serikali ya Port-au-Prince iliomba msaada wa kimataifa mwezi Oktoba, lakini licha ya wito wa mara kwa mara wa Umoja wa Mataifa, ombi hilo halikujibiwa hadi pale Kenya iliposema mwezi Julai kuwa ilikuwa tayari kuongoza Ujumbe kama huo.