1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haiti kufanya uchaguzi Agosti 2025

1 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, amedhamiria uchaguzi nchini humo kufanyika kufikia Agosti 31 mwakani, licha ya kuongezeka kwa uhalifu wa magenge yenye silaha.

https://p.dw.com/p/4d3n6
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry.
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, akihutubia kwenye Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2023.Picha: Craig Ruttle/AP Photo/picture alliance

Taarifa hiyo ilitolewa na Jumuiya ya Mataifa ya Karibiani (CARICOM?, siku moja baada ya kukamilika kwa mkutano wa kilele wa kikanda nchini Guyana.

CARICOM ilisema ingelituma timu ya usimamizi kutathmini mahitaji ya uchaguzi kufikia Machi 31 kwa ajili ya kuunga mkono masuala ya kupanga na kubuniwa kwa taasisi husika.

Soma zaidi: CARICOM: Waziri Mkuu wa Haiti kuandaa uchaguzi

Henry aliyeingia madarakani baada ya kuuawa kwa rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise, mwaka 2021, awali alikuwa ameahidi kuachia ngazi mapema mwezi wa Februari, ila baadaye akasema ni sharti kuwepo na usalama ili uchaguzi uwe huru na haki.

Waandamanaji wamejitokeza kwa makundi mitaani wakipinga tarehe hiyo iliyotangazwa naHenry.

Siku ya Alhamis (Februari 29) kulikuwa na ufyatulianaji mkubwa wa risasi katika mitaa ya mji mkuu, Port-au-Prince, huku kiongozi maarufu wa magenge, Jimmy Cherizier, akitoa wito wa kupinduliwa kwa serikali ya Henry.