1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Umoja wa Mataifa waonya kitisho kikubwa nchini Haiti

28 Septemba 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya katika ripoti ya umoja huo kwamba Haiti inazidi kutumbukia kwenye machafuko mabaya kabisa na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuisaidia kiulinzi na kifedha.

https://p.dw.com/p/4Wt8i
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres amesema Haiti inazidi kutumbukia kwenye mzozo mbaya kabisa kutokana na kujiimarisha makundi ya uhalifu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres amesema Haiti inazidi kutumbukia kwenye mzozo mbaya kabisa kutokana na kujiimarisha makundi ya uhalifuPicha: Mary Altaffer/AP/picture alliance

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwenye ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatano kwamba machafuko yanayofanywa na magenge ya uhalifu yanazidi kuongezeka, na magenge hayo yanazidi kuimarisha udhibiti hadi nje ya mji mkuu Port-au-Prince.

Amesema uhalifu unaofanywa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia unaohusisha ubakaji wa makundi, na ambao umeendelea kutumiwa na wahalifu kuwatisha raia walio chini ya udhibiti wao.

Ripoti hiyo inatolewa wakati wanachama wa Baraza la Usalama la umoja huo wakijadiliana juu ya ujumbe wa usalama wa kimataifa, ulioombwa na mamlaka za Haiti ili kulisaidia jeshi lake la polisi lenye watumishi wachache na uhaba wa rasilimali.