1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gündogan ajiunga na Barcelona kutoka Man City

26 Juni 2023

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania Barcelona, wamemsajili nahodha wa zamani wa Manchester City Ilkay Gundogan bila malipo.

https://p.dw.com/p/4T3dC
UEFA Champions League | Finale | Manchester City vs Inter Mailand | Gündogan
Gündogan akishiriki fainali ya Champions League dhidi ya IntermilanPicha: Martin Rickett/PA Images/IMAGO

Taarifa kutoka kwa klabu hiyo ya Uhispania zinasema Gündogan mwenye umri wa miaka 32 amejiunga na Barca kwa mkataba wa miaka miwili na mkataba huo utakapokwisha kutakuwa na uwezekano wa kumuongezea mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

Barcelona imesema mkataba wake una kipengee kitakachoipelekea klabu inayotaka kumnunua kulipa yuro milioni 400. Gundogan ambaye ni raia wa Ujerumani, ameondoka Manchester City baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda makombe matatu msimu uliopita, Ligi Kuu ya England, FA Cup na Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Champions League.

UEFA Champions League | Finale | Manchester City vs Inter Mailand | Gündogan
Ilkay Gündogan akilibeba kombe la Champions LeaguePicha: Dilara Senkaya/REUTERS

"Imekuwa ni fahari kubwa sana kuwa sehemu ya Manchester City kwa miaka saba iliyopita," alisema Gündogan, "Manchester imekuwa nyumbani kwangu na nimejihisi kama sehemu ya familia ya kipekee katika klabu hiyo."