1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Guterres: Taliban iondoe zuio la wanawake kuajiriwa na UN

5 Aprili 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutaka utawala wa Taliban ubatilishe maramoja marufuku yake dhidi ya wanawake wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4Pjvs
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema katika taarifa kwa niaba ya Guterres kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa haki za kimsingi za wanawake.

Guterres ameitaka Taliban kufuta hatua zote zinazozuia haki za wanawake na wasichana kufanya kazi, kupata elimu na uhuru wa kutembea.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan - UNAMA ulitarajiwa kufanya leo mazungumzo na maafisa wa Taliban kutafuta ufafanuzi kuhusu marufuku mpya ya serikali ambayo inawazuia wanawake kulifanyia kazi shirika hilo la kimataifa, kote nchini humo. Umoja wa Mataifa huwaajiri karibu wanawake 400 wa Kiafghanistan.