1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Mitandao ya kijamii na AI inazidisha chuki

26 Novemba 2024

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba mitandao ya kijamii na akili mnemba isiyodhibitiwa inazidisha misukumo mibaya zaidi ya binadamu.

https://p.dw.com/p/4nRno
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Alexander Kazakov/SNA/IMAGO

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba mitandao ya kijamii na akili mnemba isiyodhibitiwa inazidisha misukumo mibaya zaidi ya binadamu, kuruhusu matamshi ya chuki kuenea na kuchochea ghasia.

Akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Itikadi Kali (UNAOC) nchini Ureno, Guterres amesema kuna ulazima wa kusitisha kuenea kwa matamshi ya chuki na habari potofu mitandaoni.

Ameongeza kusema majukwaa ya kidijitali na akili mnemba ambayo hayajachunguzwa yamewezesha matamshi ya chuki kuongezeka kwa kasi. Australia yawasilisha muswada wa kudhibiti mitandao ya kijamii kwa watoto

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa ametumia jukwaa la mkutano huo pia kushinikiza kuwepo kwa amani Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan.