1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres kufanya ziara mpakani mwa Misri na Gaza leo

Hawa Bihoga
23 Machi 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atautembelea mpaka wa Misri na Gaza leo Jumamosi kwa dhamira ya kufufua miito ya usitishwaji wa mapigano, hatua ambayo huenda italeta ahueni kwa umma wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4e3Lg
Umoja wa Mataifa | Katibu Mkuu  Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitembelea eneo la vita, huku akizunguukwa na ulinzi mkaliPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Safari ya Guterres inafanyika katika wakati ambapo Israel inatishia kufanya operesheni kubwa ya kijeshi katika mji wa Rafah ulioko kwenye mpaka huo na Misri, licha ya miito ya kimataifa inayoitaka nchi hiyo iachane na mpango huo.

Takriban wakaazi milioni 2.3 wa Gaza wanajihifadhi katika eneo la Rafah, ingawa hali ya kiutu inatajwa kuzorota zaidi katika upande huo wa Kaskazini mwa Gaza huku mzozo ukiendelea.

Soma pia:Netanyahu: Israel itaendelea na mpango wa kuishambulia Rafah

Mbali ya mpaka huo, Katibu Mkuu huyo pia atakitembelea kitongoji cha Al Arish kaskazini mwa rasi ya Sinai nchini Misri, ambako misaada mingi ya kimataifa inahifadhiwa kabla ya kupelekwa Ukanda wa Gaza.