1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres atoa wito wa kupunguza mvutano Bahari ya Shamu

Sylvia Mwehozi
13 Januari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa pande husika kupunguza mvutano katika Bahari ya Shamu, hali inayoweza kuvuruga amani na utulivu wa kikanda.

https://p.dw.com/p/4bBwo
Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Picha: Shannon Stapleton/REUTERS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa pande husika kupunguza mvutano katika Bahari ya Shamu, hali inayoweza kuvuruga amani na utulivu wa kikanda.

Guterres ametoa kauli hiyo baada ya Marekani na Uingereza kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya waasi wa Kihouthi nchini Yemen jana Ijumaa.

Baadae, msaidizi wa Katibu Mkuu kanda ya Mashariki ya Kati Khaled Khiar, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kunashuhudiwa mzunguko wa ghasia ambao unahatarisha usalama mkubwa wa kisiasa, athari za kiuchumi na kibinadamu huko Yemen na kanda nzima.

Naye Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzya ameyataja mashambulizi hayo ya Marekani na Uingereza kuwa ni uchokozi mkali wa silaha dhidi ya nchi nyingine.