1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres alalamikia mataifa kutumia pesa katika silaha

14 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelalamikia msisitizo unaowekwa na baadhi ya serikali katika kununua silaha kwa gharama, katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliana na ongezeko la joto na njaa.

https://p.dw.com/p/4cMlF
Marekani New York | Katibu Mkuu Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya wahanga wa mauaji ya Holocaust, Machi 27.Picha: Lev Radin/Pacific Press/picture alliance

Guterres ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama uliyohusu kuhusu uhusiano kati ya chakula, mabadiliko ya tabia nchi na migogoro. Amesema inasikitisha kuona serikali zikitumia gharama kubwa kununua silaha, huku zikikabiliwa na njaa katika bajeti ya uhakika wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu zaidi.Katibu mkuu huo wa Umoja wa Mataifa alionya kwa kusema bila ya kuchukuliwa hatua hali itazidikuzorotahuku Beth Bechdol, naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, akitoa mfano wa nchi kama Burkina Faso, Mali na Niger.