1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea-Bissau yarejeshewa umeme baada ya kulipa

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Kampuni ya Kituruki ya Karpowership imerejesha umeme katika mji mkuu wa Guinea-Bissau baada ya serikali kuanza tena kulipa deni la kampuni hiyo.

https://p.dw.com/p/4XkvQ
Guinea-Bissau | Geraldo Martins, Premierminister von Guinea-Bissau
Waziri Mkuu wa Guinea-Bissau, Geraldo Martins.Picha: privat

Waziri wa Uchumi wa Guinea-Bissau, Suleimane Seidi, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano (Oktoba 18) kwamba serikali imeweza kulipa kiasi cha dola milioni 6 kati ya 15 za malimbikizo ambazo inadaiwa.

Kampuni ya Karpowership ilizima umeme katika taifa hilo la Afrika Magharibi kutokana na deni la dola milioni 17. 

Guinea Bisaau imekuwa ikitegemea kampuni hiyo ya umeme ya Uturuki kukidhi asilimia 100 ya mahitaji yake ya umeme tangu makubaliano yao ya mwaka 2019.

Mnamo mwezi Septemba, kampuni hiyo ilizima usambazaji umeme katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, kutokana na deni la takriban dola milioni 40.