1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Guardiola: Arsenal ya msimu huu ni kitisho

26 Aprili 2023

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuanza kupata mchecheto wakati kinyang'anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu ya Premia kikizidi kuwa moto.

https://p.dw.com/p/4QZya
UK Fußball Premier League | Manchester City - AFC Bournemouth | Pep Guardiola und Erling Haaland
Picha: Martin Rickett/PA Images/IMAGO

"Siku zote nilikuwa na hisia kwamba itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Arsenal katika hatua hii, hasa baada ya wao kupoteza alama muhimu katika mechi zao tatu za mwisho, itakuwa vigumu zaidi hivi sasa," ameeleza Guardiola.

Hii leo usiku, Manchester City inateremka uwanjani Ettihad kuchuana na Arsenal, mechi inayotajwa kuwa muhimu na ambayo huenda ikaamua mustakabali wa ubingwa.

Vijana wa Pep Guardiola wanasaka taji lao la tano la Premia katika muda wa siaka sita, lakini pia wako kwenye kinyang'anyiro cha kuwania mataji matatu msimu huu likiwemo Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Washika bunduki Arsenal wanaongoza jedwali wakiwa na alama 75, alama 5 mbele ya Manchester City inayoshikilia nafasi ya pili ikiwa na alama 70.

Hata hivyo Arsenal imecheza mechi mbili zaidi tofauti na mabingwa watetezi Manchester City. Timu zote mbili zinafahamu kuwa ushindi katika uwanja wa Ettihad leo utawafanya kuchukua udhibiti wa mbio za ubingwa.

Arsenal, ambayo ilikuwa inaongoza jedwali kwa alama nane mwanzoni mwa mwezi Aprili, ilishinda taji la Ligi ya Premia mara ya mwisho mnamo mwaka 2003-04.