1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Grossi awasili Iran kwa mazungumzo ya nyuklia

3 Machi 2023

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia (IAEA), Rafael Grossi amewasili Ijumaa mjini Tehran.

https://p.dw.com/p/4OEF5
Iran | IAEA-Chef Rafael Grossi zu Atomgesprächen in Teheran
Picha: dpa/XinHua/picture alliance

Grossi yuko  nchini humo kwa mazungumzo na maafisa wa Iran baada ya wakaguzi wa shirika hilo kufichua chembechembe za urani zilizorutubishwa kwa kiwango cha chini kidogo tu ya silaha za nyuklia.

Ripoti ya siri ya IAEA imesema chembechembe hizo zimefikia kiwango cha asilimia 83,7 na zinakaribia viwango vya asilimia 90 zinazohitajika ili kubuni silaha za nyuklia, ziligundiliwa katika kiwanda kilichopo chini ya ardhi huko Fordo, karibu kilometa 100 kusini mwa mji mkuu Tehran.

Ziara ya Grossi inajiri huku shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Vienna likiishinikiza Iran kuongeza ushirikiano katika shughuli zake za nyuklia.

Hata hivyo Iran inaendelea kukanusha kuwa na nia ya kuwa na silaha za nyuklia na kukanusha kufanya jaribio lolote la kurutubisha madini ya urani kwa zaidi ya asilimia 60.