1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Greta Thunberg ajiunga na maandamano ya tabianchi Uholanzi

12 Novemba 2023

Mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg amejiunga na maelfu ya waandamanaji mjini Amsterdam katika maandamano yenye lengo la kuongeza shinikizo, suala la mabadiliko ya tabia nchi liorodheshwe katika ajenda za kisiasa.

https://p.dw.com/p/4YilX
Maandamano ya wanamazingira ya Amsterdam Novemba 5, 2022
Maandamano ya wanamazingira ya Amsterdam Novemba 5, 2022Picha: Selman Aksvºnger/AA/picture alliance

Maandamano hayo yanafanyika ikiwa ni siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu nchini Uholanzi. Waandaaji wamesema maelfu ya watu wanashiriki maandamano hayo.

Utafiti unaonesha kwamba masuala muhimu yanayopewa kipaumbele katika kampeini ya uchaguzi ni mgogoro wa ukosefu wa makaazi nchini humo,viwango vya hali ya maisha pamoja na uhamiaji.

Soma zaidi: Wanaharakati wa hali ya hewa waanza maandamano makubwa

Kwa mujibu wa utafiti wa maoni uliofanywa na taasisi ya I&O suala la mabadiliko ya tabia nchi sasa halipewi umuhimu kama ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021 nchini humo.

Utafiti wa maoni ya wapiga kura pia umeonesha uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na mpambano mkali kati ya chama cha siasa za wastani za mrengo wa kati,VVD cha waziri mkuu anayeondoka Mark Rutte na chama kipya cha NSC kinachoongozwa na Pieter Omtzigt kiongozi wa mapambano dhidi ya ufisadi.