1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Green Zone ya Baghdad yashambuliwa kwa maroketi

8 Desemba 2023

Eneo lenye ulinzi mkali maarufu kama Green Zone kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambako kuna ofisi ya ubalozi wa Marekani limeshambuliwa kwa roketi kadhaa mapema leo asubuhi.

https://p.dw.com/p/4ZwRR
Afisa usalama akiulinda ubalozi wa Marekani kwenye eneo la Green Zone mjini Baghdad, Iraq.
Afisa usalama akiulinda ubalozi wa Marekani kwenye eneo la Green Zone mjini Baghdad, Iraq.Picha: Ameer Al Mohammedaw/dpa/picture alliance

Duru mbili za kiusalama za Iraq zimeeleza kuwa roketi tatu zilirushwa na kuangukia kwenye viunga vya eneo hilo, ambako pia kuna ofisi za serikali na balozi za mataifa ya kigeni.

Haikuweza kufahamika mara moja iwapo mifumo ya ulinzi ya ubalozi huo wa Marekani ilikuwa ikifanya kazi.

Soma zaidi: Mtu mmoja ajeruhiwa katika shambulio la roketi mjini Baghdad

Wakati huo huo, Marekani imeitolea wito Iraq kuwalinda wanadiplomasia wake baada ya shambulizi la roketi.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi la leo katika ubalozi wa Marekani.