1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu wanaharakati 200 wa mazingira waliuawa, 2023

10 Septemba 2024

Ripoti ya kila mwaka ya Shirika la kimataifa la Global Witness, imeeleza kuwa takribani wanaharakati 200 wa mazingira duniani kote waliuawa mwaka jana, 2023.

https://p.dw.com/p/4kTWR
Wanaharakati wa mazingira mjini Bogotá
Wanaharakati wa mazingira waliohudhuria maandamano ya Mtandao wa Hali ya Hewa Duniani mjini Bogota, Colombia mnamo Septemba 20, 2019. Wanaharakati hawa wanakabiliwa na kitisho cha kuuawa nchini humoPicha: Juancho Torres/picture alliance/AA

Colombia kwa mara nyingine inashikilia rekodi ya kuwa nchi isiyo salama kwa wanaharakati hao.

Ripoti hiyo pia imemulika ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa mazingira nchini Uingereza, Ulaya na Marekani. Kanda ya Amerika Kusini inasalia kuwa eneo hatari duniani kwa wapigania haki wa mazingira, ikiwa na karibu asilimia 85 ya mauaji 196 yaliyorekodiwa mwaka jana.

Soma pia:Safari za ndege zasitishwa Frankfurt kutokana na maandamano

Colombia, Brazil, Honduras na Mexico ndio nchi zinaongoza katika ripoti hiyo. Shirika hilo liliorodhesha vifo 79 nchini Colombia pekee.

Barani Afrika, kumerekodiwa vifo vinne pekee lakini kuna wasiwasi kuwa huenda takwimu hizo ni makadirio ya chini kutokana na changamoto ya kukusanya taarifa.