1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuAfrika

Ghala la WFP laporwa na waasi wa RSF nchini Sudan

29 Desemba 2023

Wapiganaji wa Kundi lililoaasi nchini Sudan la RSF wamepora ghala linalotumiwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP katika jimbo lililokumbwa na migogoro.

https://p.dw.com/p/4aiX5
Sudan | Ghala la chakula la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP
Ghala la chakula la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFPPicha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Shirika hilo limeeleza kuwa bidhaa zilizoibiwa wikiendi iliyopita huko al-Jazirah ikiwa ni pamoja na nafaka, mafuta na mboga za majani zingeliweza kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni wapatao 1.5. 

WFP imesema kuwa vikosi vya RSF vimepora pia lishe maalum 20,000ambazo kwa kawaida hutolewa kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo pamoja na wanawake wanaonyonyesha.

Soma pia:Kiongozi wa kundi la RSF la Sudan atembelea Uganda na kukutana na Rais Museveni

Kundi la RSF linaloongozwa na Mohamed Dagalo limekuwa likipambana na jeshi la Sudan tangu mwezi April mwaka huu (2023).