1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: idadi ya wakimbizi imezidi sana Ujerumani

30 Septemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameonesha dhamira ya kuyasaidia majimbo ya Ujerumani katika kukabiliana na wimbi la wakimbizi huku kukiwa na ongezeko kubwa la maombi ya waomba hifadhi.

https://p.dw.com/p/4X0Ta
Flüchtlinge Deutschland 2015
Picha: Markus Schreiber/picture alliance/AP/dpa

Serikali ya Berlin tayari imeanzisha ukaguzi wa mpaka na Poland na Jamhuri ya Czech. Katika mahojiano yake yaliyosambazwa leo hii amesema serikali yake ipo katika juhudi ya kuzuia uhamiaji haramu kwa kuimarisha udhibiti mipakani.Amesema idadi ya wakimbizi wanaojaribu kuingia Ujerumani ni kubwa mno kwa sasa na kuongeza kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wahamiaji hawana rekodi za usajili, ingawa karibu wote wamekuwa katika nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya.Kansela Scholz ametoa matamshi hayo huku kukiwa na kashfa ya rushwa katika mchakato wa utoaji visa nchini Poland na majaribio katika Umoja wa Ulaya kufanikisha sera ya uhamiaji ya jumuiya nzima, pamoja na hali ya ndani ya Ujerumani ya kutokuwa na sera ya maridhiano kuhusu uhamiaji.