GENEVA:Pyongyang kusitisha kabisa mpango wa nyuklia
3 Septemba 2007Matangazo
Korea Kaskazini imeahidi kutoa maelezo kamili na pia kusitisha kabisa mpango wake wa nyuklia kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Mjumbe maalum katika mazungumzo ya nyuklia ya Korea Kaskazini naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani bwana Christopher Hill amefahamisha hayo baada ya kumalizika mkutano wa siku mbili kati yake na maptanishi wa maswala ya nyuklia wa Korea Kaskazini Kim Kye-gwan mjini Geneva nchini Uswisi.
Bwana Hill ameeleza kwamba matokeo ya mazungumzo hayo ya pande mbili yatajadiliwa katika mkutano wa pande sita baadae mwezi huu.
Korea Kaskazini inatarajia kuwa uhusiano kati yake na na jamii ya kimataifa utaimarika baada ya nchi hiyo kuzingatia hatua ya kusitisha mpango wake wa nyuklia.