1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Geneva:Mazungumzo ya shirika la biashara yavunjika.

24 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4U

Mazungumzo ya dakika ya mwisho ya kuokoa makubaliano ya Doha kwa shirika la biashara la dunia yanaonekana kuvunjika.

Maafisa wa biashara walianza mazungumzo yao ya mwisho hapo jana lakini wameshindwa kufikia makubaliano yoyote baada ya majadiliano ya masaa 14.

Nchi zinazoendelea zilitarajia makubaliano hayo kuwapeleka katika manufaa mazuri katika kuendesha soko la biashara la dunia, kwa bidhaa zao.

Marekani na Ulaya kwa pamoja zinatumia mabilioni ya fedha kuendeleza kilimo cha ndani kinachokuza uchumi wa nchi zao zimesema kuwa si sawa kuvunjika kwa mazungumzo hayo kwani itasababisha bidhaa kupanda bei zaidi.