1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Wasaidizi wa MSF waachiliwa huru nchini Congo

12 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4R

Wafanyakazi 2 wa shirika la misaada la madaktari MSF,waliozuiliwa mateka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,wameachiliwa huru.Msemaji wa MSF mjini Geneva amethibitisha kuwa mfanyakazi mmoja wa Kifaransa na dreva wake wa Kicongo wameachiliwa huru na hali ya afya yao ni nzuri. Wasaidizi hao walichukuliwa mateka wiki iliyopita,walipokuwa njiani kwenda kwenye kambi ya wakimbizi katika jimbo la Ituri.Katika kipindi cha miaka sita ya nyuma,mapambano ya kikabila katika jimbo hilo karibu na mpaka wa Uganda yamesababisha hadi vifo 60,000 na zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kuhama makwao.