1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Ujerumani yampongeza Koffie Annan.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUR

Ujerumani imeipongeza hatua ya katibu wa umoja wa mataifa Koffie Annan ya kutaka kufanya mageuzi katika baraza kuu la umoja wa mataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer amevieleza vyombo vya habari huko Geneva kuwa uamuzi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffie Annan ni wa muhimu na wenye sera za kudumisha amani na utangamano katika karne ya 21.

Waziri Fischer pia alipongeza juhudi mpya za kufanyiwa mabadiliko wakala wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa.

Katika hotuba yake kwa tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu waziri Fischer aliitaka Urusi ichunguze visa vya kukiukwa kwa haki za kibinadamu katika majeshi yake huko Chechnya.

Vile vile waziri Fischer alitaja vitendo vya mateso na hukumu ya kifo nchini Iran na kuwekwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani na kuuwawa kwa watuhumiwa kwa njia zisizoeleweka nchini China.

Ujerumani iantafuta kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.