1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Niger yahitaji msaada wa dharura wa chakula

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF91

Niger iliyokumbwa na ukame imetoa wito wa kupewa msaada wa dharura wa chakula,kuwasaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,kiasi ya watu milioni 3.6 wapo katika hali mbaya sana na wanahitaji msaada.Umoja wa Mataifa umetoa muito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa Euro milioni 13 kusaidia kile kilichoitwa „msiba usiotajwa“.Nzige nchini Niger vile vile wanahatarisha zaidi uwezekano wa kupata mavuno.Familia nyingi katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi ambayo ni masikini sana,hutegemea mashamba yao kwa chakula.