1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Israel yalaumiwa kukiuka haki za binadamu

12 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDMK

Baraza la Umoja wa Mataifa linalotetea haki za binadamu,limeituhumu Israel kuhusu mashambulio yanayofanywa dhidi ya raia nchini Lebanon.Baadhi kubwa ya wanachama 47 katika baraza hilo ilipiga kura kuliunga mkono azimio linaloituhumu Israel kuwa inakiuka haki za binadamu na inavunja makubaliano ya kimataifa.Katika mkutano wa mjini Geneva,baraza hilo la Umoja wa Mataifa vile vile limetoa mwito wa kusitishwa mapigano moja kwa moja na limetoa amri ya kupeleka Lebanon ujumbe utakaochunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya Israel.